Mwakalebela adai uchaguzi wa TFF haukuwa huru na haki
Mwakalebela alipata kura tatu kwenye uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita mkoani Dodoma huku wapiga kura wakimpa ridhaa hiyo, Wallace Karia kura rais kwa kumpa kura 95, akiwaacha kwa mbali sana wapinzani wake Shija Richard, Ally Mayay waliopata kura tisa kila mmoja , Iman Madega kura nane, Mwakalebela 3 na Emmanuel Kimbe kura mmoja.
Mwakalebela aliyewahi pia kuangushwa katika uchaguzi wa TOC baada ya kupata kura 10 dhidi ya 45 za Filbert Bayi ameliambia Gazeti la Mwananchi kuwa uchaguzi wa TFF haukuwa huru wala wa haki huku akiainisha sababu nne za kwanini uchaguzi huo anaona haukuwa huru na wa haki.
“Najipanga kwa uchaguzi ujao, nitaogombea tena tukijaliwa kufika, tumeangalia mapungufu na mwisho wa uchaguzi huu ndiyo mwanzo wa uchaguzi ujao, lazima nigombee tena,” alisema Mwakalebela.
“Kwanza mchakato ulivyoanza tu, kitendo cha kuvunja kamati ya uchaguzi ilikuwa ni kinyume na katiba ya TFF kwani katiba inasema kamati inapaswa kuwa madarakani katika kipindi cha miaka miwili.
“Pili ni kitendo cha Kamati ya utendaji kukutana ndani ya siku mbili kuzungumzia uchaguzi badala ya kutoa notisi ya siku 14, tatu Simba ilipeleka mjumbe asiye sitahili kupiga kura na akapiga na uchaguzi umefanyika wakati kukiwa na rufaa ya Iringa ambayo haijatolewa majibu,” alisema Mwakalebela.
Post a Comment