MAREKANI KUPITIA SHIRIKA LAKE LA MISAADA LA USAID YAIPATIA TANZANIA DOLA MILIONI 225 KWA AJILI YA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wa kwanza kushoto) akisaini mkataba wa Makubaliano (Strategic Assistance Agreement )na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas(katikati) kuhusu utoaji wa fedha hizo dola za kimarekani Millioni 225 , tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. Wakwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson akishuhudia.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto) akibadilishana mkataba ya makubaliano (Strategic Assistance Agreement) na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto) akipiga makofi pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas(katikati), na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano (Strategic Assistance Agreement ) katika ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya kusaini mkataba huo utakaowezesha Tanzania kupatiwa fedha hizo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas mara baada ya tukio hilo la mkataba wa makubaliano katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. 

Siku moja baada ya Marekani kutangaza kutoa fedha za nyongeza katika mwaka ujao kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini,nchi hiyo imetiliana saini na Wizara ya Fedha na Mipango makubaliano ya kutoa Dola Milioni 225. 
Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Kilimo na Utawala bora. Hafla
ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini 

Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) hapa nchini Bw. Andy Karas. 
Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Bw. Doto James ameishukuru Marekani kwa kuendeleza uhusiano mzuri uliopo na Tanzania na amesema fedha hizo zitasaidia kuimarisha juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi. Nae
Bw. Andy Karas amesema Serikali na watu wa Marekani wanafurahishwa na kuendelea kwa ushirikiano mwema kati yao na Serikali ya Tanzania katika maendeleo na ameahidi kuwa ushirikiano huo utadumishwa. Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Kaimu Balozi wa
Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson ambaye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo. 

No comments

Powered by Blogger.