MAHAKAMA YAKATAA KUPOKEA MSOKOTO WA BANGI KAMA KIELELEZO KESI YA WEMA

 Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa na Mama yake Mzazi wakiingia katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwaajili ya kusikiliza mashtaka yanayo mkabili ya kutuhumiwa kutumia dawa za kulevya.
Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam wakati wakisubiri kusomewa Mashtaka yanayomkabili ya Matumizi ya Dawa za Kulevya.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo imekataa  kupokea msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka kama vielelezo vya
ushahidi dhidi ya tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya imayomkabili Wema Sepetu na wenzake.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi
Mkuu,Thomas Simba ambaye amesema mahakama haiwezi kupokea vielelezo
hivyo kwa sababu vina kasoro.

Akitoa uamuzi wake amesema anakubaliana na hoja zilizotolewa  na upande wa mashtaka kwamba msokoto wa bangi na vipisi hivyo vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua mahakamani.Kesi hiyo imeahirishwa hadi September 12/2017.

No comments

Powered by Blogger.