KESI YA WEMA KUUNGURUMA LEO
KESI inayomkabili mlimbwende wa Bongo Movie, Wema Sepetu ambaye anatuhumiwa kwa matumizi ya bangi imeahirishwa kusikilizwa kwa muda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kutokana na wakili anayemtetea kutokuwepo mahakamani hapo.
Wema aliyefika mahakamani hapo akiwa ameambatana na mama yake mzazi, Mariam Sepetu na watuhumiwa wenzake, alichoieleza mahakama kuwa wakili wake ameshindwa kufika kwa wakati kutokana na majukumu mengine kwani anasikikiza kesi nyingine inayoendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Thomas Simba alipotaka kuiahirisha hadi siku nyingine, wakili wa serikali aliiambia mahakama kuwa anaomba kesi hiyo isikilizwe leo kutokana na shahidi upande wa serikali ambaye ni mkemia kuwepo kwa siku ya leo na kuanzia kesho anatarajia kusafiri.
Hivyo hakimu aliisogeza mbele kesi hiyo hadi saa 6:30, leo mchana ambapo wakili wa Wema anatarajiwa kuwa ameshawasili mahakamani hapo.
Post a Comment