HAJI MANARA: NIYONZIMA MMOJA TU NI SAWA NA WACHEZAJI 10 WA YANGA

Siku chache kabla ya pambano la Ngao ya Jamii kati ya Yanga dhidi ya Simba, tambo zimeendelea ambapo safari hii Simba wameendelea kutoa tambo dhidi ya wapinzani wao hao wa jadi.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ndiye ambaye amehusika safari hii kwa kutoa kijembe kikali kwa Yanga kuhusu suala zima la usajili ambao Simba wameufanya.
Manara amesema kuwa kwa usajili ambao wao Simba wameufanya ni mkubwa na hakuna klabu inayofikia thamani ya usajili wao.
Amedai kuwa ukiwakusanya wachezaji waliosajiliwa Simba thamani yao ni kubwa kuliko wachezaji wote ambao wamesajili katika timu nyingine zote za Ligi Kuu ya Vodacom 
Msemaji huyo mwenye maneno mengi ya kisoka, ameenda mbali zaidi kwa kusema kitendo cha Simba kumsajili Haruna Niyonzima kina maana kubwa na kudai kuwa thamani yake ni kubwa kiasi cha kufananisha thamani ya Niyonzima ni sawa na wachezaji 10 wa Yanga. 

No comments

Powered by Blogger.