HAJI MANARA: MECHI YA YANGA, TUTAANZISHA WACHEZAJI TISA UWANJANI
Kuelekea mchezo dhidi ya Yanga, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa anatamani mchezo huo dhidi ya wapinzani wao hao wa jadi uchezwe hata kesho, lakini kuna kubwa zaidi ya hilo amelitamka.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii ambapo unazikutanisha timu bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na bingwa wa Kombe la FA ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa msimu wa 2017/18.
Akizungumza katika mahojiano asubuhi ya jana jijini Dar es Salaam, Manara amesema Simba ipo tayari na kikosi chao kipo fiti kuelekea mchezo huo kiasi kwamba wanajiandaa kuanzisha kikosi cha wachezaji tisa uwanjani badala ya 11.
Manara amesema raha ya mchezo huo ni presha iliyopo lakini mchezo huo ukimalizika kila mtu atakuwa kimya kwa kuwa kwa sasa kuna kelele nyingi mitandaoni.
Akizungumza zaidi Manara alisema: “Ingawa kanuni zinaruhusu kuwa na wachezaji 9 lakini tutawaomba TFF waturuhusu kuanzisha wachezaji tisa hivi, ili kuwarahisishia na mambo kama ya kadi nyekundu, nafikiri tutawaandikia barua kuwaomba hilo.”
Post a Comment