AMBER ROSE NA HEKAHEKA ZA KUPUNGUZA MATITI
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanamitindo huyo ambaye yu mapenzini na mwanamuziki 21 Savage, aliposti picha inayoonyesha kifua chake vizuri na kuomba ushauri kwa mashabiki wake juu ya mpango wake wa kuyapunguza matiti yake.
“Ninafikiria kuyapunguza matiti yangu mwaka huu, matiti yangu ni makubwa sana na mazito yananisababishia maumivu ya mgongo, nashindwa hata kuvaa baadhi ya nguo bila sidiria, lakini naogopa nikifanya oparesheni ya kupunguza matiti nitabaki na makovu.
“Naomba ushauri jamani, kuna mwanamke yeyote aliyewahi kupunguza matiti yake na anaishi maisha ya furaha pamoja na kubaki na makovu? Naomba mniibie siri, hivi wanayapunguzia kwenye chuchu au wapi, mwenye uzoefu naomba aniambie,” ameandika Amber Rose.
Post a Comment