RUVUMA: VIONGOZI WA CHEDEMA WALIOKAMATWA, WAACHILIWA HURU

                                          Viongozi wa Chadema (Picha na Maktaba).

NYASA, RUVUMA: Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji, wabunge wawili wa chama hicho na viongozi wenzao saba wa chama waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushikiliwa tangu juzi wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma wameachiliwa huru leo.
Afisa Habari wa Chadema Tumaini Makene amethibitisha kuachiliwa kwa viongozi hao.
Waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi hilo ni Katibu Mkuuwa chama hicho,  Vincent Mashinji, mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na Mbunge wa Viti Maalumu, Zubeda  Sakuru kwa kile kilichoelezwa kuwa ni maagizo aliyopewa ODC wa Nyasa.
Wengine ni
1. Philbert Ngatunga (Katibu wa Kanda)
2. Ireneus Ngwatura (M/kiti Mkoa)
3. Delphin Gazia (Katibu Mkoa)
4. Zubeda Sakuru (Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma)
5. Asía Mohamed (Afisa Kanda)
6. Cuthbert Ngwata (M/kiti Wilaya)
7. Charles Makunguru (Mwenezi Wilaya)
Baada ya kukamatwa, juzi Jumamosi, Julai 15, viongozi hao walipelekwa kituoni kuhojiwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao walivamia kikao cha ndani cha Chadema kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Dk Mashinji ya kukagua shughuli za chama katika kanda hiyo.

No comments

Powered by Blogger.