Rais Magufuli kuwatimua viongozi wa mikoa na wilaya zitakazokumbwa na njaa

Rais John Magufuli amesema Serikali haitatoa chakula kwa mkoa utakaokumbwa na baa la njaa na badala yake viongozi wa mkoa huo watawajibishwa.

Ameyasema hayo leo Jumanne, Julai 25 wakati wa ziara yake ya uzinduzi wa barabara na kuongeza kuwa kiongozi ambaye hatahamasisha watu wake kulima hafai kuwa kiongozi.

“Wilaya ikiwa na njaa nitajua wewe mkuu wa mkoa hufai, mkuu wa wilaya hufai. Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya atakayeshindwa kuwahamasisha watu wake wafanye kazi, hafai kuwa kiongozi,” amesema.

Amewataka wakuu wa mikoa kuwaondoa katika nafasi zao makatibu tarafa ambao hawahamasishi kilimo.

“Ikiwezekana na wewe mkuu wa wilaya au mkoa, kama unakaa kijijini au ni katibu kata onyesha mfano wako wa kazi. Ukiwa diwani, hivyo hivyo, ukiwa mbunge hivyo hivyo.  Ndiyo maana ninatimiza wajibu wangu wa kuhamasisha watu, chapa kazi, hapa kazi tu.” Amesema.

No comments

Powered by Blogger.