Mbio za walemavu Majimaji Selebuka 2017 zageuka gumzo


                                       Bingwa wa mbio za walemavu 21km, shukuru halfan.
mshindi wa pili mbio za walemavu, John Stephano 

     Bingwa wa walemavu, shukuru halfan kulia akimsapoti mshindi wa pili, john stephano 

         Bingwa wa walemavu, shukuru halfan kulia akimsapoti mshindi wa pili, john stephano 
        Mshindi wa kwanza wa mbio za walemavu 21km,shukuru halfan akipokea medali yake.
 Mshindi wa pili wa mbio za walemavu 21km, John stephano akivikwa medali Luteni Kanali Bumalo
Washindi wa km 21 wa Tamasha la Majimaji Selebuka, wakiwa na mkuu wa kikosi cha makao makuu ya bligedi, Luteni Kanali Bumalo. kulia ni mshindi wa pili, Stephano, bingwa Halfan na mshindi wa tatu, Jolo

 Mwandishi Wetu, Songea
Hamasa kwenye tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka inazidi kupaa juu, hii ni kutokana na mwitikio chanya unaozidi kujionesha mwaka hadi mwaka, na mwaka huu mbio za walemavu ‘paralympic’ za 21km ndiyo imekuwa gumzo.
Ushiriki wao umetajwa kama chagizo kubwa la watazamaji kurundikana kwenye Uwanja wa Majimaji ambako hakuna kiingilio huku wengi wakionekana kuwapa hamasa tangu mwanzo wa mbio mpaka wanakabidhiwa tuzo, wengi wakiwapongeza kwa ujasili wao wa kuvuta pumzi kwa kilomita 21.
Katika mchuano huo wa kuwania kitita cha laki nne kwa bingwa, Jumapili Julai 23, kitita hicho kilitwaliwa na Shukuru Halfan aliyetumia muda wa dakika 18:13, nafasi ya pili ikichukuliwa na John Stephano aliyetumia muda wa  1:56:32 na kupewa laki tatu na mshindi wa tatu alikuwa Mathias Jolo kwa muda wa 2:08:39 na kuondoka na laki mbili.
Aidha katika jumla ya orodha ya washiriki wa mbio hizo, Halfan alishika nafasi tisa akiwapiku wengi wasio na ulemavu licha ya yeye akiwa na ulemavu wa mkono mmoja. Stephano ana upungufu wa mikono yote wakati Jolo ni mlemavu wa mguu.
Katika mahojiano maalum, Halfan amesema: “Kuna dhana ya walemavu kutojiamini katika kujaribu jambo, lakini kupitia tamasha hili kuwashauri wenzangu wawe na moyo wa uthubutu na kujiamini kama wanaweza kazi yoyote sawa na wasio na walemavu. Angalia, nimeshika nafasi ya tisa katika jumla ya washiriki 15, jiulize nimewapiku wazima wangapi?”
Stephano ni mlemavu wa mikono yote, huku Halfan akikosa kiungo cha mkono mmoja na Jolo ni mlemavu wa mguu.

No comments

Powered by Blogger.