MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA 2017

Kikundi cha ngoma aina ya Mganda kutoka Luhagala kikifanya yake kwenye mashindano ya ngoma za asili ya Tamasha la Majimaji Selebuka2017, linaloendelea Uwanja wa Majimaji, mjini Songea.
 Kikundi cha ngoma Boma Ruhagala aina ya Kioda  katika mchuano wa kusaka bingwa wa ngoma za asili katika Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
 Baadhi umati waliofurika kushuhudia mchuano mkali wa ngoma za asili katika Tamasha la Majimaji Selebuka.
 Mmoja wa wateja akipata huduma ya bure katika banda la Polisi Ruvuma ambao ni washirika wakuu katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2017. Huduma zitolewazo ni  elimu juu ya madawa ya kulevya, usalama barabarani, dawati ya jinsia ya watoto.
                                                      wajasiriamali nao awakubaki nyuma
                                            Nmb bank nao walikuwepo kutoa huduma za kibenki. 

Katika muendelezo wa tamasha la majimaji selebuka linaloendelea kwenye uwanja wa majimaji mjini songea, ruvuma jana jumatatu ilikuwa ni mashindano ya ngoma za asili ambazo zitafanyika kwa siku mbili. tamasha hilo iloanza kutimua vumbi julai 23, litahitimishwa julai 30, mwaka huu kwa kushuhudia mbio za baiskeli za 100km kutoka wilaya ya mbinga- songea mjini. washindi katika mbio hizo atapata shavu la kupata kozi ya kimataifa ya mchezo huo kati ya afrika kusini. ​

No comments

Powered by Blogger.