Picha: Masanja Mkandamizaji alivyokutana na Majeruhi wa Lucky Vicent nchini Marekani
Emmanuel Mgaya, Maarufu kama Masanja Mkandamizaji akiwa nchini Marekani amekutana na kuzungumza na watoto Sadia na Wilson ambao ni majeruhi ya ajali ya shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha wanaopatiwa matibabu nchini humo.
Masanja pia kupitia ukurasa wake wa instagram amethibisha kukutana na watoto hao:
WAZAZI WAO WANAWASALIMU NA WANAWASHUKURU KWA USHIRIKIANO NA MAOMBI YENU..MUNGU AMENIPA NEEMA YA KWENDA KUWAONA WADOGO ZETU WALIOPATA AJALI SADIA NA WILSON NA KUWEPO MAREKANI KWA MATIBABU….. IMEKUWA SIKU NJEMA KWETU SOTE TUMEFURAHI PAMOJA NAO KULA NAO NA KUMTAFAKARI MUNGU KWA PAMOJA.
LAKINI PIA NIMEZUNGUMZA NA WENYEJI WAO WALIOFANIKISHA SAFARI YA WAO KUJA MAREKANI!! HAKIKA MUNGU NI MWEMA WAMEENDELEA KUIMARIKA NA WANAENDELEA VIZURI!!
SHUKRANI KWA MADAKTARI NA KILA ALIYETENGA MDA WAKE KUWAOMBEA!!
Picha: Mtandao
Post a Comment