Magufuli atikisa Tamasha la Majimaji Selebuka


 Mkurugenzi mwenza wa Asasi ya Somi, Julian Murchison, akimkabidhi tuzo mwakilishi wa Kikundi cha Ngoma ya Mganda, Gerodi Kiwili, kilichoibuka bingwa wa mashindano ya ngoma za asili kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka 2017.
 Balozi wa tamasha la majimaji selebuka na mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, akimkabidhi tuzo mwakilishi wa kikundi cha ngoma ya kioda, Anjela Mhagama.
 Mwakilishi wa kikundi cha ruvuma champion, Issa Mkwawa kilichoshika nafasi ya pili akipokea tuzo kwa Mohamed Kaunda 'mchele'.
 Washindi wa ngoma za asili katika picha ya pamoja. Kutoka kulia ni mwakilishi mshindi wa tatu kikundi cha ngoma ya kioda, Anjela Mhagama, mwakilishi wa mabingwa, kikundi cha Mganda, Gerodi Kiwili na Issa Mkawa mwakilishi wa mshindi wa pili, kikundi cha ruvuma champion.
 kikundi kilichoibuka bingwa wa  ngoma za asili katika picha ya pamoja na viongozi wa tamasha la majimaji
Kikundi cha ngoma ya kioda kilichoshika nafasi ya tatu kikiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa tamasha la majimaji selebuka linaloendelea mjini songea.
        kikundi cha ruvuma champion kikiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa tamasha
Kikundi cha Ruvuma Champion kikiwasha moto katika fainali ya mashindano ya ngoma za asili. Kimeshika nafasi ya pili.

Na Mwandishi Wetu
KASI ya awamu ya tano chini ya Amri Jeshi Mkuu, Dkt John Pombe Magufuli imezidi kutikisa kila kona ya nchi, huku wananchi wakizidi kummwagia sifa kede kede.
Ndivyo ilivyokuwa kwenye tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka linaloendelea kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, ambako vikundi karibu vyote vya ushiriki jumbe zao zilihusu ubora, ufanisi wa awamu yake ya utawala.
Mashindano hayo ambayo yalidumu kwa siku mbili na fainali kufanyika Jana Jumanne, Julai 25, mwaka huu yalishuhudiwa Kikundi cha Mganda kutoka Luhagala kikiubuka na ushindi na kujinyakulia kombe na kitita cha laki nne.
Aidha kwa kiasi kikubwa kikundi hicho kilibebwa zaidi na ujumbe wa nyimbo zao katika kuisifia serikali ya Tanzania awamu ya tano kama vile inavyopambana na ufisadi, wala rushwa, kutokomeza biashara ya madawa ya kulevya huku wakimalizia kwa msemo wa HAPA KAZI TU

No comments

Powered by Blogger.