MAAJABU YA DUNIA: AFANYIWA UPASUAJI WA UBONGO HUKU AKIPIGA GITAA


                      Abhishek Prasad (picha ya kushoto) akifanyiwa upasuaji.

ABHISHEK PRASAD mwenye umri wa miaka 37 ambaye alifanyiwa upasuaji katika ubongo wake wakati akipiga gitaa, hivi majuzi ameonyesha maajabu hayo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Bengaluru nchini India ambapo alipona tatizo lililokuwa limeviathiri vidole vyake vya mkono wa kushoto visiweze kufanya kazi yake kimailifu wakati wa kupiga chombo hicho.
Tatizo alikokuwa nalo Prasad katika ubongo wake ndilo lilisababisha hali hiyo na hivyo madaktari katika Hospitali ya Bhagwan Mahaveer Jain walipendekeza afanyiwe matibabu ya aina hiyo ambayo huwakumba wanamuziki hususan wanaotumia mikono katika kucheza zana zao.
                                                               Abhishek akitumbuiza.

Hivyo, Julai 11 mwaka huu, Prasad alikuwa akipiga gitaa lake wakati madaktari walipochimba kishimo kwenye kichwa chake ili kufanya tiba hiyo na ambapo mgonjwa huyo alikuwa anajitambua kikamilifu katika mchakato mzima.
 Akizungumza na vyombo vya habari baada ya upasuaji huo, Prasad alielezea kitendo hicho cha kipekee cha kujitambua wakati akifanyiwa upasuaji huo uliochukua saa saba huku vidole vyake vikitembea kwa umahiri katika mpini wa gitaa.
                                      Akionyesha eneo alilofanyiwa upasuaji.

“Sikuzikia maumivu yoyote kwani walikuwa wamenidunga dawa za kienyeji za ganzi sehemu ya upasuaji,” alisema. “Tulimtaka awe analipiga gitaa wakati wa upasuaji kwani alikuwa na matatizo ya vidole wakati tu anapiga chombo hicho,” alisema Dk. Sharan Srinivasan, aliyefanya upasuaji huo na akaongeza:
                                         Akipiga gitaa wakati wa upasuaji.                      
 “Wakati anapiga gitaa, ndipo tuliweza kubaini tatizo lenyewe na kulipatia tiba.” Nyuzi alizoshonewa Prasad ziliondolewa Alhamisi iliyopita ambako aliwashukuru madakatari na kuwapigia nyimbo kadhaa kuonyesha alivyopona.

No comments

Powered by Blogger.