CHUO CHA MUSLIM MOROGORO WATOA FURSA YA WATANZANIA KUSOMA LUGHA YA KICHINA
Mkufunzi wa Lugha ya Kichina Sun Fei akielezea jambo kwa mwanafunzi aliyefika katika banda la Chuo cha Muslim Morogoro namba ya kujiunga na Chuo chao na kusoma elimu ya lugha ya Kichina. Picha na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Afisa Habari wa Chuo cha Muslim Morogoro Ngaja Mussa akitoa maelezo wa wageni waliotembelea banda la Chuo hicho na kuwaelezea namna wanavyofanya udahili wa wanafunzi kwa mwaka 2017/18 pamoja na elimu ya lugha ya Kichina inayopatikana katika chuo chao kwenye Maonesho ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Wanafunzi akitoa maelezo wakati walipotembelea banda la Chuo hicho na kuwaelezea namna wanavyofanya udahili wa wanafunzi kwa mwaka 2017/18 pamoja na elimu ya lugha ya Kichina inayopatikana katika chuo chao kwenye Maonesho ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MAONESHO ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yamefunguliwa rasmi leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Kassim Majaliwa Kassim huku yameonesha mwitikio mzuri kwa vyuo mbalimbali vilivyojitokeza kudahili wanafunzi wanaotaka kujiunga na kozi tofauti kwenye vyuo vyao.
Ili kutoa fursa ya elimu kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo, Chuo cha Muslim Morogoro kimewataka wanafunzi wachangamkie fursa ya elimu ya lugha ya Kichina inayopatikana katika chuo chao kwani kimeweza kuwasaidia wanafunzi wengine kufahamu lugha hiyo pamoja na kupata nafasi za kusoma nchini China bure.
Akizungumza na Globu ya Jamii, Afisa Habari wa Chuo cha Muslim Morogoro Ngaja Mussa amesema kuwa wanatoa kozi ya elimu hiyo ya lugha ya kichina kwa wanafunzi wote wanaotaka kuifahamu na pia utakaposoma kwa mwaka mmoja na kuifahamu vizuri lugha hiyo unapata nafasi ya kusoma nchini China.
Ngaja amesema kwa sasa kuna walimu takribani saba wanatoa mafunzo ya elimu hiyo katika chuo chao, mbali na kozi hiyo ya lugha ya Kichina wanatoa pia kozi mbalimbali katika ngazi ya astashahada, stashahada na shahada.

Kwa ngazi ya shahada kwa mwaka 2017/18 wana kozi za Bachelor of Arts with Education pamoja na Bachelor of law with Shariah huku ngazi ya Astashahada na Stashahada wana kozi za Procurement and Logistics Management, Journalism, Medical Labaratory Technology, Science and Laboratory Technology, Laws with Shariah pamoja na Islamic Bankinga and Finance.
Post a Comment