BOMOABOMOA KIMARA YAANZA BARABARA YA MOROGORO

 Baadhi ya waathirika wakiondoa vifaa mbalimbali katika nyumba zilizobomolewa.
 Zoezi likiendelea la waathirika kukusanya na kuokoa kile walichodhani kitawafaa.
                                        Taswira ya eneo ambalo zoezi hilo limefanywa.
BAADHI ya wakazi wa Kimara-Stop Over jijini Dar es Salaam leo walipatwa na taharuki baada ya bomoabomoaya nyumba zilizojengwa katika hifadhi ya Barabara ya Morogoro ilipoanza leo  mchana.
Waathirika wa tukio hilo waliozungumza na mtandao huu  walitoa wito kwa Rais John Magufuli aingilie ili kusitishwa kwa  zoezi hilo kwani walisema nyumba walizojenga sehemu hiyo zilikuwa haziko katika hifadhi yabarabara wakati huo.

No comments

Powered by Blogger.