HIVI NDIVYO DAVID BECKHAM ALIVYOFURAHIA MAISHA YA TANZANIA AKIWA NA FAMILIA YAKE
Video fupi inayomuonyesha staa huyo akiwa na familia yake wakitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, ilithibitisha kuwa alikuwa nchini Tanzania japokuwa baadaye ilielezwa kuwa alikuwa ni kwa ajili ya masuala yake binafsi.
Katika picha ambazo Beckham ambaye ni staa wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na timu ya taifa ya England amezitupia katika ukurasa wake wa Instagram ameonekana akiwa na furaha katika Mbuga ya Serengeti.
Aidha katika ukurasa wake huo, Beckham ameweka video fupi inamuonyesha akiwa mbugani na kusha kumuona simba, katika maelezo ya video hiyo ameandika kuwa hilo ni jambo zuri na linavutia.
Katika ujio huo, Beckham amekuja na mkewe na watoto wake wanne.
Post a Comment