MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA YAKAMATA KONTENA MBILI ZA KEMIKALI BASHIRIFU
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya imekamata kontena mbili zilizobeba kemikali bashirifu zilizokuwa tayari kwa kuingizwa nchini katika eneo la Bandari Kavu ya Ami Tabata Relini, Jijini Dar es salaam.
Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Kulevya , Rogers Siang’ a ameendesha operesheni ya ukamataji wa Kemikali bashirifu ambazo zilikuwa zikiingia nchini na kuanza kwa matumizi yake.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kemikali hizo, Kamishna Msaidizi wa Ukaguzi wa Kemikali Jinai , Bertha Mamuya, amesema mzigo huo ni mwendelezo wa mzigo wa kampuni ya Tecno Scientific ambayo ilikuwa ikifanyia shughuli zake katika eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.
Amesema hapo awali waliweza kukamata lita 10,000 za Kemikali Bashirifu na katika Bandari ya Dar es Salaam zaidi ya lita 6000 zimekamatwa zikitokea nchini Ufaransa.
Ametaja kuwa mamlaka inaendelea na uchunguzi wa kuzichunguza kemikali hizo hili kubaini kama zimefuata njia sahihi ya kuingia nchini na iwapo itabainika kuwa Kemikali hizo zimeingia kinyume cha sheria wahusika watapelekwa mahakamani.
Post a Comment