BREAKING NEWS :HANS POPPE AREJEA SIMBA, NI BAADA YA KUMALIZANA NA UONGOZI
Zacharia Hans Poppe, amereja Simba.
Uamuzi wa Hans Poppe kurejea Simba umetokana na mkutano uliofanyika hadi saa 9 usiku wa kuamkia leo.
Hans Poppe amethibitisha kurejea kwake kundini baada ya mkutano huo na viongozi.
Hans Poppe aliamua
kujiondoa katika kamati ya utendaji ya Simba na akawa akawa ametoka
kwenye kamati ya usajili aliyokuwa mwenyekiti.
Lakini kikao hicho hadi saa 9 alfajiri usiku wa kuamkia leo, kimemaliza suala hilo na Hans Poppe ameamua kurejea.
“Kweli tumekutana
hadi saa 9 usiku, mwisho tumekubaliana na tumeyamaliza vizuri. Huu ni
wakati wa kusonga mbele,” alisema Hans Poppe.
Post a Comment