Jambazi Lauawa Kwa Kupigwa Risasi Jijini Dar

Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na askari katika jaribio la kupora fedha.
 
Watu walioshuhudia tukio hilo lililotokea  jana Jumapili wamesema mtu huyo akiwa na wenzake walijaribu kupora fedha  kwenye gari kabla ya kuwekwa kwenye mashine ya kielektroniki ya kutolea fedha (ATM) ya benki moja iliyopo katika jengo la makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar.
 
“Aliyekufa aliamriwa asipite barabara hii, alipokataa kusimama polisi walipiga risasi hewani, naye alipotaka kutoa bastola ndipo polisi walipomfyatulia risasi na alikufa papo hapo,” amesema shuhuda wa tukio hilo na kuongeza kuwa
wengine waliokuwa na mtu huyo walikimbia na mmoja amekamatwa.
 
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema atazungumzia tukio hilo leo

No comments

Powered by Blogger.