Askofu Gwajima Ataja Njia Mbadala ya Kuwabaini Wahusika wa Mauaji Kibiti
Askofu
Gwajima
Askofu wa Kanisa la Ufufuo
na Uzima, Josephat Gwajima amesema Serikali inapaswa kuwashirikisha
viongozi wa dini katika kupambana na mauaji ya Polisi na raia
yanayoendelea kutokea katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani
Pwani.
Akihubiri katika Ibada ya Jumapili
jana kwenye kanisa lake lililoko Ubungo jijini Dar es Salaam, Askofu
Gwajima alisema mauaji hayo ni roho kamili ambayo pamoja na sheria za
nchi, inapaswa kuondolewa kwa maombi.
Alifafanua kuwa Jeshi la Polisi
nchini na dola wanazuia uhalifu kimwili, lakini viongozi wa dini
wanazuia ki roho, hivyo wote wanatakiwa kushirikiana ili kukomesha
matukio hayo ya mauaji yanayoleta hofu kwa watu.
“Kiongozi wa dini anaweza kwenda
Kibiti na kuwaambia walioua polisi na kuendeleza mauaji wajitokeze na
kusalimisha silaha na wakaja, lakini watu hao wakiitwa na Polisi walete
silaha hawatatokea,’ alisema.
Akitumia mfano wa mahubiri aliyosema
kuwa aliwahi kuyatoa mwaka 1995 eneo la Kibiakali, Gwajima alisema
viongozi wa dini wana nguvu ya ziada kupambana na uhalifu.
“Mimi nimewahi kuhubiri mwaka 1995
huko Kibiakali na kusema kuwa waliokuwa wanamiliki silaha walete kwa
jina la Yesu na nilifanikiwa kukusanya SMG nane ambazo walileta kwa
mikono yao,” alieleza.
“Hivyo, tunaomba (viongozi wa dini) Serikali itupatie nafasi ya kuhubiri ili kuweza kupambana na roho hizo za mauaji. Pia huu ni wakati wa Kanisa kulia na kusali ili kuweza kupambana na vita hivi vya kiroho ambayo inahitaji nguvu ya rohoni kukamata wahalifu.
“Hivyo, tunaomba (viongozi wa dini) Serikali itupatie nafasi ya kuhubiri ili kuweza kupambana na roho hizo za mauaji. Pia huu ni wakati wa Kanisa kulia na kusali ili kuweza kupambana na vita hivi vya kiroho ambayo inahitaji nguvu ya rohoni kukamata wahalifu.
Katika hatua nyingine Askofu Gwajima alisema Tanzania ni nchi iliyobarikiwa, hivyo siyo vyema watu wakaitabiria mabaya.
Ameyasema hayo jana wakati wa Ibada
ya Jumapili kanisani kwake Ubungo. Alisema kuna jambo ambalo Mungu
atafanya ambalo litaonyesha dhahiri kuwa Tanzania ni nchi tajiri.
“Watanzania ni makuhani wa nchi,
tumezaliwa nchi hii tumekunywa maji katika nchi hii, hivyo hatupo radhi
kuona watu wanatabiri vitu ambavyo havipo katika utabiri.”
Aliendelea “Wiki iliyopia nilisema
baadhi ya watu ambao walikuwa wanafanya Tanzania shamba la bibi kwa
kila mtu kuilani nchi hii, wanatakiwa kujua kuwa Tanzania ni nchi
iliyobarikiwa.
Pia itafika wakati mataifa yatajua
kuwa nchi hii ni tajiri hivyo viongozi wa dini na waumini wanatakiwa
kuiombea ili mpango wa Mungu uweze kutimia.
“Na ndio maana hivi karibuni
nimekuwa mkali kwa baadhi ya manabii wanaotabiri mabaya katika Taifa
hili sipo radhi kuona watu wanatabiri mambo ambayo hayaendani na nchi
hii kwani hivi karibuni Mungu atajidhirisha katika nchi hii ambayo ipo
kwa makusudi yake”alisema.
Aliongeza kuwa wapo watu ambao
wataona aibu nchi hii siku ambayo Mungu atajidhihirisha na kuiweka juu,
hata hivyo waumini na viongozi wanatakiwa kuitabiria mema nchi na
kuiombea ili baraka zake zishuke.
“Mungu alimwambia Sauli toka
uende, na utakapokuwa unakwenda utakutana na manabii watakao kuwa
wanatabiri roho ya Bwana atashuka na kuwa mtu mwingine, Leo hii waumini
mbalimbali wametoka sehemu tofauti na kuja kusikia utabiri huu. Sisi ni
mabalozi wa Mungu hapa duniani.
Alifafanua kuwa Kanisa halitakiwa
kulilia demokrasia bali linatakiwa kulilia Ufalme kwamba ule ushawishi
wa mbinguni Mungu akisema ndio hakuna wa kupinga, bali mtafuata tu hata
kama wengi wanasema lakini watafuata tu.
Baadaye sheria ijae Katiba ya Mungu, Sheria ya Mungu na tusimame katika mlima Kilimanjaro na kutangaza neema na ufalme wa Mungu.
Gwajima alisema wanasiasa hawaaminiki
na kuwataka Watanzania kuweka tumaini lao kwa Mungu ambaye ndiye
anayeweza kuwapa msaada wa kweli.
“Unafikiri wanasiasa wanaweza
kuibadili nchi? Je, una mtazamo huo? Ukimtembelea mwanasiasa mmoja na
mwingine ni kama leo unamtembelea chui na kesho simba. Usiweke tumaini
juu yao, weka tumaini lako kwa Mungu”
chanzo globalpublishers.co.tz
chanzo globalpublishers.co.tz
Post a Comment