Mbowe Atinga Mahakamani Sakata la Madawa

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, leo amefika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kufuatilia mwenendo wa kesi ya kikatiba aliyoifungua dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Camilius Wambura.
Katika kesi hiyo,  mbali na mambo mengine, Mbowe anapinga amri ya Makonda ya kutaka akamatwe na pia kile alichokiita kudhalilisha watu wakati mkuu huyo wa mkoa alipotaja majina ya watu.
Kesi imeendelea kunguruma na ilibidi iahirishwe mpaka saa saba mchana ambapo walipoingia mahakamani kwa mara nyingine,  Mahakama Kuu imekubali maombi ya mawakili wa Mbowe kwamba asikamatwe hadi tarehe Februari 23, mwaka huu kesi itakaposikilizwa tena.

No comments

Powered by Blogger.