Waliofukiwa na kifusi mgodini Geita, waokolewa
Wakipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuokolewa.
Watu 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ mkoani Geita wameokolewa wakiwa hai
Watu 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ mkoani Geita wameokolewa wakiwa hai
Tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano ya
wiki iliyopita ambapo jitihada za kuwaokoa zilikuwa zikifanyika kwa
takriban siku 4 mfululizo mhadi siku ya jana ambapo waokoaji
walifanikiwa kucharanga mwamba na kupata upenyo uliowezesha mawasiliano
kati ya waokoaji, na watu hao.
Zoezi limekamilika leo majira ya saa 5:02 asubuhi na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.
Zoezi hilo limeshuhudiwa na Naibu Waziri
wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani pamoja na Mkuu wa mkoa wa
Geita, Meja Jenerali Ezekiel Kyuga.
Mara baada ya zoezi hilo kukamilika,
watu pamoja na wanahabari waliokuwepo katika eneo hilo walionekana
kulipuka kwa shangwe na kuwapokea wahimbaji hao ambao kati yao
walikuwemo wenye uwezo wa kuongea ambao walisimulia tukio lilivyokuwa
pamoja na kusema kuwa walikuwa wamajawa na hofu wakiamini kuwa
wasahaulika.
Awali kabla ya kuokolewa, yalifanyika
mawasiliano ya kuwatumia ujumbe kwa kutumia waya ili waseme wako wangapi
na majina yao, ambapo walisema kuwa wako 15 na kwamba walikuwa na njaa
na walihitaji maji, soda, uji n.k
Hizi ni baadhi ya picha na
zinazoonesha zoezi la uokoaji lilivyokuwa ambapo watu hao akiwemo raia
wa China wamepatiwa huduma ya kwanza na kisha kupelekwa hospitali kwa
uchunguzi zaidi.
Taarifa zaidi zitakujia kadri zinavyotufikia........
Post a Comment