ULIMWENGU AENDA KUKAMILISHA MCHONGO KUKIPIGA LIGI YA SWEDEN
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu, anaondoka
nchini leo kuelekea nchini Sweeden kwaajili ya kukamilisha usajili wake
katika klabu ya Ligi Kuu ya nchini humo, AFC Eskilstuna.
Katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, Ulimwengu amesema kuwa
mazungumzo yamekamilika na sasa anakwenda kusaini mkataba wa miaka
miwili na klabu hiyo.
“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa watu wote waliofanikisha
suala hili, kama Jamal Kisongo ambao wamekuwa karibu na mimi kwa kipindi
chote hiki na kunipa ushauri hadi kufikia maamuzi haya ya kujiunga na
timu hii. Tumekataa ofa nyingi sana na kuikubali hii kwa sababu za
msingi sana,”alisema.
Ulimwengu alisema kwamba anashukuru Mungu ndoto zake za kucheza Ligi
Kuu Ulaya zinatimia na ataitumia AFC Eskilstuna kama daraja la kupandia
timu kubwa barani humo.
“Kila kitu ni malengo tu, inategemea na mtu unataka kitu gani katika
wakati gani, nakwenda AFC Eskilstuna kucheza mpira kama nilivyocheza TP
Mazembe ili nionekane nisogee mbele zaidi,”alisema.
Ulimwengu menye umri wa miaka 23 aliibukia katika taasisi ya soka
Tanzania (TSA) mwaka 2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa
Ligi Kuu katika klabu ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi
mwaka 2010 alipokwenda akademi ya Athletic FC ya Sweden, alikocheza hadi
2011 TP Mazembe alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe.
Alicheza U-20 ya Mazembe kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi
timu ya wakubwa mwaka 2012 na moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha
kwanza hadi anamaliza Mkataba wake Oktoba mwaka jana.
Ulimwengu anajivunia kushinda mataji makubwa akiwa na Mazembe kama
Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na pamoja na kucheza Klabu
Bingwa ya Dunia. Habari kwa hisani ya Bin Zubeiry
Post a Comment