Simbachawene, DC Ilala: Wamachinga Waondoke Haraka Kwenye Barabara za Mwendokasi January 25, 2017
Bi. Mjema ndiye alikuwa wa kwanza.
“Nitoe wito wangu kwa wamachinga
wote wanaofanya shughuli zao kandokando ya barabara za mabasi haya ya
mwendokasi walioko maeneo ya Msimbazi, Kariakoo na kwingineko katikati
ya jiji la Dar es Salaam waondoke wenyewe, kuelekea kwenye maeneo
waliyotengewa ambayo moja wapo ni Lumumba.
Hatuwezi kuwavumilia kuendelea
kuleta usumbufu, kufanya biashara barabarani, ajali zisizo za lazima.
Hawa ni Watanzania wenzetu tunawapenda, wasifikiri kwamba hatuwezi
kuwagusa, tunawaomba waondoke kabla hatujawaondoa sisi wenyewe.” Alisema Mjema.
Simbachawaene akafuatia
Naye Waziri wa Tamisemi, George
Simbachawene ameongeza kuwa wmachinga wanaofanya biashara zao kwenye
njia za waenda kwa miguu waondoke mara moja kwani wanavunja sheria na
kusababisha madhara na hata watembea kwa miguu kugongwa na magari na
kufa.
“Ninatoa agizo kwa wamachinga wote
wanaofanya biashara wenye njia za wtembea kwa miguu waondoke waende
kwenye maeneo rasmi waliopangiwa.
Barabara hizi zimejengwa kwa ajili
ya usafiri, magari, pikipiki, na pebeni ni baiskeli na watembea kwa
miguu na siyo kwa ajili ya watu kuwea biashara zao.
“Wanaovuka kwa miguu wamekuwa
wakipata ajali na kufariki kutokana na wamachinga kubana barabara kwa
kufanya biashara zao na kusababisha adha hiyo kwa watembea kwa miguu.
“Nimemuagiza Mkuu wa mkoa wa dar es salaam, paul Makonda alishughulikie suala hilo haraka iwezekananvyo.” Alisema Simbachawene.
Post a Comment