RAIS DONALD TRUMP KUDHIBITI RAIA WA MATAIFA KADHAA YA KIISLAM KUINGIA MAREKANI

Rais wa Marekani Donald Trump anaanza leo kutekeleza mipango kuhusiana masuala ya usalama wa taifa hilo ikiwemo kutangaza kujenga ukuta katika mpaka baina ya Marekani na Mexico.

Trump atatia saini maagizo yake kadhaa kuhusiana na masuala ya uhamiaji na usalama wa mipaka katika siku kadhaa zijazo, ikiwemo kuzuia kuingia Marekani watu wanaotokea kwenye mataifa kadhaa ya Kiislam.

Agizo hilo la rais linalenga kusitisha utoaji viza kwa raia wa mataifa ya Sudan, Irak, Iran, Libya, Somalia, Syria na Yemen, pamoja na kufanyiwa mchujo wa hali ya juu watu kutoka katika mataifa ya Kiislam.

No comments

Powered by Blogger.