Mtoto wa Mbunge Anaswa Usiku na Golikipa Timu ya Mtibwa Sugar
Dar es Salaam: Binti wa
aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM), Naima Shaa amezua
balaa kwa mara nyingine baada ya kunaswa akijiachia kwa mapozi ‘tata’ na
golikipa namba moja wa Timu ya Mtibwa Sugar, Saidi Mohamed ‘Nduda’.
Tukio hilo lililoacha gumzo kwa muda lilijiri katika Ukumbi wa Maisha Basement, Kijitonyama, Dar ambapo wawili hao walikuwa wamekwenda kustarehe.Kwa kamera ya shushushu wetu, Nduda alifika ukumbini hapo akiwa na washkaji zake na Naima naye alikuwa kivyake lakini walipokutana hali ilibadilika na kuanza kufan
“Walionesha kama watu waliomisiana
kitambo. Nduda alipomuona Naima tu, alimfuata harakaharaka na kuanza
kupiga naye mapicha tata kabla ya kukumbatiana na kuzungumza kwa muda
huku wengine wakisema kuwa ni mrithi wa aliyekuwa mpenzi wa mwanadada
huyo ambaye ni kipa wa Simba, Peter Manyika Jr,” alifunguka shushushu wetu na kuongeza:
Naima Shaa akiwa na Manyika JR“Baada ya kujiachia kwa mapichapicha, wawili hao walipoulizwa kama kwa sasa ni wapenzi hawakuwa tayari kufunguka
Naima ambaye aliwahi kuwa mke wa mfanyabiashara wa jijini Dar, Mwanamboka, aliwahi kuripotiwa kumzidi kete aliyekuwa shosti wake, Wema Isaac Sepetu na kudaiwa kumpora kigogo wake aliyekuwa maarufu kwa jina la CK.Mbali na hilo, pia aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ hadi kujichora tatuu ya msanii huyo. Baada ya kuachana na Dogo Aslay, Naima alitumbukia kwenye penzi la Peter Manyika Jr kabla ya uhusiano wao kukata kamba miezi kadhaa iliyopita.
Naima Shaa akiwa na Dogo Aslay.
Post a Comment