Baada ya Bilicanas na Shamba, Serikali ‘Yakamata’ Hoteli ya Mbowe wilayani Hai, Kilimanjaro
Ikiwa ni takribani miezi mitano
sasa tangu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe alipoondolewa
katika jengo la Bilicanas lililokuwa pia na ofisi za Free Media na siku
moja tangu serikali imzuie kuendeleza shughuli za kilimo kwenye shamba
lake, kiongozi huyo amepata pigo jingine katika hoteli yake
anayoimiliki.
Uamuzi
huu wa serikali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umekuja siku moja
tangu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa alipotangaza kusitisha
shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa
na Mbowe kwa madai kuwa lipo katika eneo la chanzo cha maji cha Mto
Weruweru.
Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni amepewa siku 14 na serikali awe amelipa kodi ya
hoteli yake ya Aishi takribani TZS milioni 13.5 vingine vyo hoteli hiyo
itafungwa.
Hoteli ya Aishi inayomilikiwa na Freeman Mbowe iliyopo Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mujibu
wa taarifa alizozipata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,
Freeman Mbowe amekuwa akikwepa kulipa kodi kwa miaka mitano na
kusababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato.
Kwa miaka mitano imeelezwa kuwa Mbowe
hakupeleka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hali ya mauzo yake ambayo
inapaswa kutumika kujua ni kodi kiasi gani anatakiwa kulipa.
Kuhusu shamba lake, DC alisema kuwa
shughuli za kilimo katika eneo hilo limepeleka uharibifu wa mazingira
huku kiongozi huyo akivuna miti ya asili bila kibali cha Mkuu wa Wilaya
kinachotolewa baada ya uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).
Post a Comment