Sehemu Ambazo Kamwe Huruhusiwi Kuzitembelea Hapa Duniani

 Najua kwamba ungefurahi sana kuona ukiizunguka dunia unavyotaka, utembelee fukwe zote duniani, hoteli na sehemu nyingine nyingi. Labda unasema kwamba kuna siku ukipata pesa utafanya starehe kwa kutembelea sehemu mbalimbali ili kuendelea kuona uumbaji wa Mungu.
 Ndugu yangu, nakutakia mafanikio mema lakini kumbuka kwamba hata uwe na pesa kiasi gani, kuna sehemu ambazo hutotakiwa kutembea, ni hatari na sehemu nyingine ni kwa sababu serikali haitaki wewe kutembea huko.
Hizi ni sehemu ambazo KAMWE HURUHUSIWI kutembelea hata kama utakuwa na kiasi kikubwa cha fedha. Tiririka mwanangu!
                                                                KISIWA CHA NYOKA
Hiki ni kisiwa kilichokuwa nchini Brazil, kina msitu mkubwa na kina nyoka wengi kuliko sehemu yoyote duniani. Watu wengi wamekuwa wakikatazwa kutembelea kisiwa hicho kutokana na hatari kubwa iliyokuwepo huko na hata wale watu ambao wamekuwa wakienda huko kisiri wamekuwa wakifa kwa kuumwa na nyoka hao hatari.
                                                       DEVICE ASSEMBLY FACILITY
Hii ni sehemu iliyopo nchini Marekani ambayo hutumika kutengenezea mabomu ya nyuklia zaidi ya elfu moja na kuyajaribia huko. Hata ukiangalia ardhi yake haipo na muonekano mzuri kutokana na mabomu hayo ya nyuklia ambayo yamekuwa yakijaribiwa kila siku.
Serikali ya Marekani imewakataza watu kwenda huko kutokana na hatari iliyokuwepo na hata wale wanaoishi huko ambao ndiyo watengenezaji wakubwa wa mabomu hayo wamekuwa wakiishi kwa tahadhari kubwa.
                                                      MAKUMBUSHO YA VATICAN
Ukienda nchini Vatican ambapo ndipo makao makuu ya Kanisa la Roma, kuna sehemu ambayo ndiyo uhifadhi nyaraka mbalimbali za siri, za miaka mingi nyuma na hata zile za kipindi hiki.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kutembelea huko, kuna ulinzi mkali ambao umekuwa kwa saa ishirini na nne. Kinachowafanya watu kutoruhusiwa kuingia huko ni wizi, wanahofia watu wanaweza kuingia na kuiba au kuchoma moto nyaraka hizo ambazo zimekuwa muhimu sana.
                                                                CHUMBA CHA MALKIA
Unaweza ukashangaa lakini ndiyo ukweli. Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia katika chumba cha Malkia wa Uingereza, Elizabeth II zaidi ya baadhi ya wanafamilia na yeye mwenyewe.
Kwa nje, chumba hicho kina ulinzi mkubwa, askari wamekuwa wakitembea kuhakikisha hakuna mtu anayeingia japokuwa mwaka 1982, mtu aitwaye Michael Fagn alifanikiwa kuingia na ilipogundulika, haraka akatolewa na kupelekwa polisi.
                                                              CHUMBA NAMBA 39
Hiki ni chumba cha siri nchini Korea Kaskazini. Chumba hicho ndicho chenye siri kubwa juu ya mabomu ya nyuklia yanayotengenezwa huko. Hakuna mtu ambaye anaruhisiwa kutembelea huko zaidi ya rais mwenyewe, Kim Jong-un na baadhi ya wakuu wa jeshi kwani kumejaza siri kubwa ambazo kama zitagundulika basi wanaweza kupigwa muda wowote ule.
                                                                          CHERNOBYL
Hii ni sehemu ndogo nchini Ukraine. Tarehe 26/4/ 1986 kulikuwa na ajali mbaya ya bomu la nyuklia ambalo lilijilipua huko. Maji yakaathirika, ardhi na vitu vingine.
 Hakuna mtu anayeishi huko kwa sasa na yeyote anayetaka kutembelea ni lazima aombe ruhusa kutoka katika serikalini na hata kwenda huko, hupewa mavazi maalumu kwani mpaka leo hii ile sumu ya nyuklia bado ipo.

No comments

Powered by Blogger.