Wadaiwa Sugu Bodi ya Mikopo Baso Siku 30 Tu!
Dar es Salaam: Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa
bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa hadi sasa kuna jumla ya wadaiwa
sugu 142,470 wenye mikopo ya shilingi 239,353,750,170.27 iliyokwishaiva
hawajajitokeza wala kuanza kulipa mikopo yao.
Akitolea ufafanuzi wa maana ya neo
“Wadaiwa Sugu”, Badru amesema kuwa ni wanufaika waliokopeshwa, muda wa
matarajio ukapita bila kuwasilisha taarifa zao na kulipa madeni ya
mikopo waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/1995.
Kuhusu hatua zinazochukuliwa na bodi
hiyo, Badru amesema mbali na kutoa siku 30, bodi hiyo inakamilisha
taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa kuvunja sheria ya bodi ya mikopo
kifungu cha 19A(1).
Hatua nyingine ni pamoja na
kuyawasilisha majina hayo katika taasisi za mikopo, kuwasiliana na
wadhamini wao pamoja na kuyatangaza hadharani majina ya wadaiwa sugu
wote ili waajiri, wadhamini na wadau wengine wayajue na kutoa taarifa
katika bodi hiyo.
Kuhusu takwimu za mikopo iliyotolewa,
amesema tangu 1994/95 hadi 2015/16 jumla ya shilingi 2,595,932,575.56
zimekopeshwa kwa jumla ya wanufaika 379,179.
Amesema kati ya mikopo yote
iliyokopeshwa, mikopo iliyoiva ni shilingi 1,425,708,285,046.48 kwa
wanufaika 238,430 ambao tayari wamemaliza kipindi chao cha matazamio.
Badru amesema kuwa jumla ya wanufaika
wa mikopo 93,500 wamebainika na kupelekewa ankara za madeni yao, ambapo
kati yao wanufaika 81,055 wanaendelea kulipa.
Post a Comment