Waziri Mkuu wa Congo DRC Ajiuzulu na Balaza Lake

DRC: Waziri Wkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Augustin Matata Ponyo, amejiuzulu na kutoa fursa ya kuteuliwa mrithi wake kuongoza serikali ya mpito.
Kujiuzulu kwa bwana Ponyo ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita kati ya serikali ya Rais Joseph Kabila na baadhi ya vyama va upinzani ya kuhairisha uchaguzi wa urais hadi mwezi Aprili mwaka 2018.
Wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa mhula wake wa mwisho.
Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.
Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu na bwana Ponyo.
“Nimeamua kujiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu pamoja na baraza lote la mawaziri ili kutekeleza maazimio yaliyomo kwenye barua ya makubaliano ya mwezi Oktoba,” Amesema Augustin Matata Ponyo mbele ya umati akiwepo rais Kabila.
Matata aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2012, amesema serikali imefanya mambo mengi mazuri na yenye thamani yanayoleta picha nzuri ya ukuaji wa uchumi.

No comments

Powered by Blogger.