RONALDO AFUNGA MAWILI NA KUKOSA PENATI URENO IKISHINDA

     Cristiano Ronaldo akiachia shuti na kufunga goli kwa mkwaju wa penati
          William Carvalho akifunga goli la pili la Ureno kwa mpira wa kichwa
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amefunga magoli mawili na kukosa penati wakati Ureno ikiifunga Latvia 4-1 katika mchezo wa kuwania kutinga michuano ya kombe la dunia wa kundi B.

Cristiano Ronaldo alifunga goli lake la kwanza kwa mkwaju wa penati lakini akakosa penati nyingine baada ya mapumziko baada ya shuti lake kugonga mwamba.

Arturs Zjuzins aliisawazishia Latvia kwa shuti la chini, lakini William Carvalho akaongeza la pili kwa Ureno. Ronaldo alipachika goli la tatu na baadaye Bruno Alves akakamilisha la nne.

No comments

Powered by Blogger.