Naibu Waziri wa Afya Anasa Kiwanda cha Viroba FEKI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, akiwa ameongzana na timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama wameendesha operesheni kali ya kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam  na kufanikiwa kukama shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo  hayo.

Katika operesheni hiyo, pia wamefanikiwa kukibaini kiwanda bubu kinachotengeneza kinywaji aina ya konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza Jijini Dar  es Salaam. 
Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia ‘spirit’ ambayo inachanganywa na ‘gongo’; spirit, gongo, chupa tupu na zilizojazwa, vizibo, vifungashio vimekamatwa.Kwa hatua hiyo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na polisi mpaka sasa kwa tuhuma za kuendesha shughuli hizo.
 Naibu Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akikagua baadhi ya pombe kali katika moja ya duka alilolikamata lililopo mwenge Dar es salaam wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea nchini.
 Baadhi ya pombe kali aina ya konyagi na amarula ambazo ni feki zilizokamatwa katika duka la kuuza pombe kali lililopo manzese jijini Dar es salaam wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea nchini.
Naibu Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla wa kwanza kulia akiwa ameshika beseni lililojaa vizibo vya konyagi katika kiwanda feki kilichokamatwa maeneo ya sinza Dar es salaam wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea nchini kushoto ni Afisa kutoka TFDA.

No comments

Powered by Blogger.