HARRY KANE AREJEA DIMBANI NA KUINYIMA ARSENAL USHINDI

Harry Kane amerejea tena dimbani baada ya kuwa majeruhi na kuisawazishia Tottenham goli na kuifanya timu hiyo kuwa timu pekee ambayo haijafungwa katika Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya kutoka sare ya 1-1 na Arsenal.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza alikuwa benchi tangu aumie Septemba 18, aliifungia Tottenham kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha pili baada ya Kevin Wimmer kujifunga katika kipindi cha kwanza.
 Harry Kane akipiga mpira wa penati uliozaa goli la kusawazisha la Tottenham
 Homa ya mchezo huo ilipanda na kuamsha ghadhabu kama inavyoonekana hapa

No comments

Powered by Blogger.