LIVERPOOL YAFANYA KUFURU NA KUKWEA KILELENI MWA LIGI KUU YA UINGEREZA
Sadio Mane aliifanya Liverpool
iongoze kwa kufunga kwa mpira wa kichwa cha sarakasi, baada ya
wenyeji hao kukosa nafasi kadhaa, na kisha baadaye Philippe Coutinho
kufunga la pili kwa shuti la umbali wa yadi 20.
Adam Lallana alimdondoshea krosi
Emre Can na kufunga goli la tatu kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili
kilipoanza Roberto Firmino aliunganisha kimiani pande la Lallana
kabla ya Mbrazili huyo kumtengenezea goli Mane na kisha Georginio
Wijnaldum kutikisa la sita.
Msenegal Sadio Mane akiruka kichwa cha sarakasi na kufunga goli la kwanza Roberto Firmino akiifungia Liverpool goli la nne katika mchezo huo
Post a Comment