Wafungwa wakosa sare, Walazimika kukaa Uchi Gerezani mkoani Katavi

Imebainika kuwa wafungwa wa Gereza la Kalilankulukulu lililopo wilayani Tanganyika mkoani Katavi licha ya kukosa sare za wafungwa Gerezani na kuwasababishia kukaa Utupu, wafungwa hao pia wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama
Hali hiyo inawasababishia pia kutembea kwa miguu kwa umbali mrefu wa kilometa 10 kuyatafuta maji
Hayo yamesemwa na mkuu wa gereza hilo Samwel Obete Lulu wakati akitoa taarifa kwa mbunge wa viti maalum Mkoani Katavi Tasika Mbugo pindi alipotembelea gereza hilo kwa ajili ya kuzungumza na wafungwa
Mbali na changamoto hiyo wafungwa hao hulazimika kulia chakula mikononi badala ya vyombo maalum
Mbunge huyo amejitoa kwa kuwakabidhi shilingi 336,000/= kwa ajili ya kununua vikombe, bakuli na sabuni za kuogea
Mkuu wa wilaya hiyo Salehe Mhando amemshukuru mbunge huyo kwa moyo wake wa kujitolea huku akiiomba wizara ya mambo ya ndani ya nchi kuliangalia suala la wafungwa wa gereza hilo na kulitatua kwani linakiuka haki za binadamu 

chanzo:edwinmoshi.blog

No comments

Powered by Blogger.