SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA GENK KUITWANGA BILBAO MABAO 2-0 EUROPA CUP




KRC Genk imeonyesha si timu ya mchezo baada ya kuitwanga Athletic Bilbao
ya Hispania kwa mabao 2-0 katika mechi ya Europa Cup.
Genk iliyokuwa nyumbani, ilipata bao katika kila kipindi huku Mtanzania
akiingia katika kipindi cha pili, ilikuwa dakika ya 56 na kuchangia
kupatikana kwa bao la pili.
Bao la kwanza lilifungwa na Jakub Brabec aliyeunganisha pasi safi ya
Leon Bailey katika dakika ya 40, wakaenda mapumziko wakiwa wanaongoza.
Samatta aliingia kuchukua nafasi ya Thomas Buffel katika dakika ya 56 na
kaanza kuonyesha cheche.
Dakika ya 83, Onyinye Ndindi alifunga bao la pili na kushindilia msumari
wa mwisho kwa Wahispania hao.
Bilbao ni kati ya timu zenye historia ya juu katika La Liga kwa kuwa ni
kongwe na haijawahi kuteremka daraja kutoka La Liga. Nyingine ambazo
hazijawahi kuteremka ni Real Madrid na Barcelona tu.


No comments

Powered by Blogger.