Kikosi Kazi Cha Jeshi La Wananchi (JWTZ) Cha Wasili Kagera Kwa Ajili Ya Kujenga Miundombinu Iliyoathiriwa Na Tetemeko La Ardhi
Kikosi
kazi cha jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)kutoka makao makuu ya
Jeshi kimewasili Mkoani Kagera kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya
serikali iliyoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoana
Kagera septemba 10 mwaka huu.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha
Kabambyaile Kata ya Ishozi Wilaya ya Missenyi, Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu alisema kuwa kikosi hicho
kina wataalamu wa fani zote za ujenzi na wamekuja na vifaa vyote vya
ujenzi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu(mwenye
Suti)akisikiliza maelezo juu ya kikosi kazi cha askari waliokuja kujenga
miundo mbinu ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi
"Hiki
kikosi kitafanya kazi kwa masaa 24 yaani watajenga usiku na mchana
taasisi zote za umma zilizoathiriwa na tetemeko ikiwa ni pamoja na
mashule na zahanati ili watoto waende shule na wagonjwa waendelee kupata
matibabu"alisema.
Alisema
mpaka kufikia july mwakani ujenzi wa miundombinu utakuwa umekamilika
kwa robo tatu na aliwataka wananchi wawape ushirikiano maeneo yote
watakayopita kujenga miundombinu ya umma.
Kiongozi
wa kikosi hicho Meja Buchadi Kakura alisema kuwa kikosi hicho kimekuja
Kagera kusaidia serikali ya Mkoa kurudisha miundombinu yote ya umma
iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi katika hali yake ya kawaida.
"Ni
vigumu kusema lini tutakamilisha ujenzi ila sisi tutafanya kazi usiku
na mchana ili ujenzi huu ukamilike ndani ya muda mfupi"Alisema Meja Kakura.
Post a Comment