Rais Magufuli aongoza mamia Ya Wananchi kumuaga Dk Masaburi
Baadhi
ya Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kichama wakiongozwa na Rais Dkt
John Pombe Magufuli (wa tano kulia) wakiwa katika viwanja vya Karimjee
mapema leo asubuhi kutoa heshima ya mwisho na kuaga mwili wa Marehemu
Dkt Didas Masaburi,aliyefariki wiki iliopita katika hospitali ya Taifa
ya Muhimbili.
Sanduku lililobea mwili wa Marehemu Dkt Masaburi likiwasili katika
viwanja vya Karimjee,jijini Dar kwa ajili ya kutolewa heshima za mwisho
Baadhi ya waombolezaji wakisubiri kuaga mwili wa mpendwa wao Dkt Didas Masaburi.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama na serikali pamoja na
wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa
Marehemu Dkt Masaburi,mapema leo viwanja vya Karimjee,jijini Dar Es
Salaam.
Rais
John Magufuli leo ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam
kuuga mwili wa aliyekuwa meya wa jiji hilo, Dk Didas Masaburi
aliyefariki Jumatano iliyopita na kusema Masaburi ana wake wanne au
watano na watoto zaidi ya 20.
Kauli
ya Dk Magufuli ameitoa muda mfupi baada ya msomaji wa wasifu wa Dk
Masaburi kusema kuwa ameacha mke mmoja waliyefunga naye ndoa Jannet
Masaburi na wajane wawili kauli ambayo ilizua miguno kutoka kwa
waombolezaji.
Alipopewa nafasi ya kuzungumza Dk Magufuli alisema anamfahamu Dk Masaburi kuwa alikuwa na wake wanne au watano hivi.
Alisema hata watoto anafahamu kuwa anao zaidi ya 20.Rais Magufuli alisema Masaburi alikuwa rafiki yake,ndugu yake na mpiganaji mwenzake ndani ya CCM.
Post a Comment