Mkuu wa wilaya aagiza kuwekwa ndani kwa Mhandisi wa manispaa
Mkuu
wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ameagiza kuwekwa ndani kwa Mhandisi wa
manispaa ya Kinondoni na baadhi ya viongozi wengine wa Kata ya
Mikocheni akiwemo mtendaji wa kata ya mikocheni kwa muda wa saa 24
kutokana na kukiuka baadhi ya maagizo ambayo serikali imekuwa ikiyatoa
ikiwemo ujenzi wa barabara ambazo zimekuwa mbovu kwa muda mrefu.
Katika
ziara ya kutembelea kata zilizopo katika wilaya ya Kinondoni kwa lengo
la kutambua kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu na
wananchi.
Mkuu
wa wilaya amefikia uamuzi huo wa kumuweka ndani mhandisi wa manispaa ya
Kinondoni Abdul Digaga ambaye hakuwepo katika ziara hiyo kitendo
ambacho mkuu wa wilaya amekitafsiri kama dharau na kisha atoe maelezo ya
kwa nini barabara mbovu zimekuwa hazitengenezwi kwa muda mrefu na
kusababisha kero kubwa kwa watumiaji ikiwemo barabara ya viwandani na
ile ya viongozi katika mtaa wa Sewa zilizopo kata ya Mikocheni.
Mbali
na hilo mkuu wa wilaya ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa kata ya
Mikocheni kutafuta eneo na kuanza ujenzi wa zahanati ya kata hiyo ambao
haujatekelezwa kwa miaka miwili sasa licha ya serikali kutoa fedha
zilizoombwa na viongozi wa kata hiyo kwa ajili ya ujenzi wa zahanati
kiasi cha shilingi Mil. 42 kwa madai kuwa wamekosa eneo la kujenga.
Post a Comment