Masikitiko: Wafanyakazi wa Serikali wachomwa moto mpaka kufa
Watu
watatu wakiwamo watafiti watatu na dereva wa Kituo cha Utafiti wa
udongo na maendeleo ya ardhi Seliani mkoani Arusha wameteketezwa kwa
moto wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Katika
tukio hilo lililotokea jana saa 12:30 jioni katika Kijiji cha Iringa
Mvumi, gari walilokuwa wanatumia aina ya Toyota Hilux mali ya kituo
hicho, lilichomwa moto.
Kabla
ya kuchomwa moto, watafiti hao mmoja kati yao mwanamke, walivamiwa na
wanakijiji cha Iringa Mvumi waliwakatakata kwa mapanga na silaha za jadi
kisha kuwachoma moto hadi kufa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha hilo na akasema atatoa taarifa za tukio hilo baadaye.
Taarifa
za awali zilizopatikana zimesema chanzo cha tukio hilo ni mwanamke
mmoja wa kijijini hicho kupiga yowe kuashiria kwamba ameona watu ambao
anahisi ni wanyonya damu (mumiani).
Taarifa hizo zilipofika kijijini, ndipo wanakijiji wakaenda kuchoma gari na kuwaua na kuwachoma moto.
Baada ya tukio hilo, Polisi walituma makachero na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walifika kijijini hapo na kuanza msako mkali.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Mvumi.
chanzo edwinmoshi.blog
Post a Comment