Manji Atangaza Rasmi Kuahirisha Mkutano Wa Yanga

 Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusufu Manji akitoa tamko lake kwa wanahabari (hawapo pichani).
                                                Mkutano na wanahabari ukiendelea.
                Baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga waliofika kwenye mkutano huo.

 Baadhi ya wanachama wakimzingira mmoja wa watangazaji wa kituo cha redio cha jijini Dar
  kutaka kutoka eneo la klabu ya Yanga kwa madai ya kutangaza tofauti na wanavyotaka wao.
 
MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji ameahirisha mkutano wake na wanachama wa klabu hiyo uliotarajiwa kufanyika kesho Jumapili kufuatia kupokea barua ya zuio la mkutano huo kutoka kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wanachama wawili wa klabu hiyo Juma Magoma na aliyewahi kuwa mwansheria wa klabu hiyo, Frank Chacha ndiyo walioiomba mahakama hiyo izuie mkutano huo uliopangwa kufanyika kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani jijini Dar.
Manji ametoa tamko hilo la kuahirisha kwa mkutano huo limetolewa leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo na kudai kuwa hawezi kuingilia uhuru wa mahakama kwani anaamini suala hilo litaisha na atatangaza tarehe nyingine ya kufanyika kwa kwa mkutano huo mara baada ya taratibu zote za kimahakama kukamilika.
Aidha Manji amewataka wanachama wa klabu hiyo kuwa wavumilivu huku akiwaomba wanachama waliokuwa watokee mikoani kuacha kuja jijini Dar es Salaam hadi hapo atakapotangaza upya.
Habari Picha: Denis Mtimana Musa Mateja/Gpl

No comments

Powered by Blogger.