LIONEL MESSI AONYESHA KUWA AMEPOANA SASA KWA KUTUPIA 'HAT-TRICK'

Mchezaji nyota duniani Lionel Messi amefunga magoli matatu 'hat-trick' wakati Barcelona ikiiadhibu Manchester City iliyobakia na wachezaji 10 dimbani kwa magoli 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alirejea Nou Camp na kuonyesha kumiliki mpira vizuri katika kipindi cha kwanza lakini baadaye wakafanya makosa mengi, yaliyopelekea kupata kipigo hicho.

Messi alipata goli la kwanza baada ya Fernandinho kuteleza na kisha baadaye Kevin de Bruyne akapoteza mpira na kumpa fursa Andres Iniesta kutoa pande kwa Messi akitumia mguu wake wa kushoto kufunga la pili.

Kipa wa Manchester City alitolewa nje kwa kudaka mpira nje ya boksi dakika chache baadaye Messi tena akaongeza la tatu. Bacelona nao walijikuta wakibakia 10, baada ya Jeremy Mathieu kupewa kadi ya pili ya njano dakika 15 kabla ya mpira kuisha.
              Lionel Messi akipiga mpira uliozaa goli la kwanza la Barcelona
Kocha Pep Guardiola akishikilia kichwa kusikilizia maumivu ya kipigo alichopata kutoka kwa timu yake ya zamani ya Barcelona

No comments

Powered by Blogger.