MESUT OZIL AFUNGA 'HAT-TRICK' YAKE YA KWANZA ARSENAL IKIUWA

 Mesut Ozil amefunga magoli matatu 'hat-trick' ya kwanza kabisa katika maisha yake ya soka wakati Arsenal ikiifundisha soka timu ya Ludogorets Razgrad katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ulioishia kwa ushindi wa magoli 6-0.



Katika mchezo huo Sanchez alifunga goli la kwanza kwa kuudokoa mpira ndani ya boksi, kisha Theo Walcott akafunga la pili kwa mpira wa kuzungusha naye Alex Oxlade-Chamberlain kufunga la tatu kwa mpira uliokuwa unazagaa zagaa.
                Alexis Sanchez akipiga mpira uliozaa goli la kwanza la Arsenal
                    Mpira uliopigwa kiufundi na Sanchez ukitinga wavuni

No comments

Powered by Blogger.