EFM Yamfikisha Kortini Paul James, Yamdai Fidia ya Tsh. Milioni 200
DAR ES SALAAM: Mtangazaji mahili wa Kituo cha Redio cha Clouds FM, Paul
James ‘PJ’ amefikishwa katika Mahakama ya Kazi yaa jijini Dar es Salaam
na Kituo cha Redio cha EFM kwa madai ya kuvunja mkataba kinyemela.PJ aliondoka EFM mwanzoni mwa mwezi
Oktoba na kurejea Clouds FM alikokuwa akifanya kazi kabla ya kuondoka
pamoja na mtangazaji mwenzake Gerald Hando.
EFM imefungua mashtaka katika Mahakama ya Kazi jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka mkataba wa kazi na kituo hicho.
Kufuatia mashtaka hayo, EFM inadai fidia ya pesa kiasi cha Tsh. Milioni 200 kutoka kwa mtangazaji huyo.
Inadai PJ alikatisha mkataba kiholela na
kurudi tena Clouds FM bila kufuata makubaliano pamoja na sheria
alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga nacho.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 23, 2016 katika Mahakama ya Kazi ya jijini Dar es Salaam.
Post a Comment