JPM Amuapisha Mama Anna Mghwira Kuwa RC wa Kilimanjaro na Kumkabidhi Ilani ya CCM
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Elisha Mgwira akisoma hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa umma mara baada ya kuapishwa Ikulu, Dar.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Anna Elisha Mgwira akiongea jambo la shukrani mara baada ya kuapishwa na Rais Magufuli kushika wadhifa huo.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Anna Elisha Mgwira akiongea jambo la shukrani mara baada ya kuapishwa na Rais Magufuli kushika wadhifa huo.
Baada ya kumuapisha, Rais Magefuli alipata nafasi ya kumzungumzia RC huyo mpya. |
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara) Ndg. Rodrick Mpogolo akimkabidhi ilani ya CCM Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akiingia kwenye gari lake kuelekea kituo chake cha kazi baada ya kuapishwa leo na Rais Magufuli.
IKULU, DAR: Rais Magufuli amemuapisha Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Bi. Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, leo Juni 6, 2017 na kumkabidhi Ilani ya CCM.“Mimi huwa siteui watu hivi hivi, naangalia uwezo wa mtu, wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi.”
“Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu.
“Kumekuwa na minong’ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo.
Post a Comment