BONDIA TONY BELLEW AMDUNDA BJ FLORES NA KISHA KUMTAKA DAVID HAYE

 
Bondia Tony Bellew, ametetea taji lake la dunia WBC kwa kumdunda kwa KO BJ Flores katika raundi ya tatu, na kumtaka David Haye kupambana naye.

Bondia huyo Muingereza Bellew alimdondosha Mmarekani BJ Flores mara tatu kwa kutumia ngumi yake kali ya mkono wa kushoto katika raundi ya pili, Jijini Liverpool.

Baada ya kumdunda JB Flores, Bellew alianza kupaza sauti za kumtaka Haye apande ulingoni huku akimponda jambo ambalo karibu lisababishe mabondia hao kuzipiga.
    Tony Bellew akimtwanga ngumi nzito ya mkono wa kushoto JB Flores
 JB Flores bondia ambaye ni rafiki wa David Haye akianguka chini baada ya ngumi kumuingia vilivyo
  Bondia Tony Bellew akimpiga mkwara bondia David Haye mwenye afro
 Bondia Tony Bellew akishuka ulingoni kumfuata David Haye ili wazichape

No comments

Powered by Blogger.