WANAWAKE WA MANCHESTER CITY WATWAA UBINGWA WA SUPA LIGI

Timu ya Wanawake ya Manchester City imeshinda kwa mara ya kwanza kombe la Supa ligi, baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya wanawake wa Chelsea.

Katika mchezo huo wa jana timu ya wanawake ya Manchester City ilihitaji sare tu ili imelize kinara wa ligi hiyo.

Kapteni wa Chelsea Katie Chapman alijifunga kufuatia shinikizo kutoka Jill Scott na kujikuta akitumbukiza kwenye lango lake kona ya iliyopigwa na Toni Duggan, kisha baadaye Duggan kufunga la pili.
                            Wanawake wa Manchester City wakifurahia ubingwa

No comments

Powered by Blogger.