VIONGOZI WAKUU 70 DUNIANI WAHUDHURIA MAZISHI YA SHIMON PERES

Rais Barack Obama amemwagia sifa marehemu Shimon Peres na kumlinganisha na hayati Nelson Mandela, Malkia wa Uingereza pamoja na viongozi wengine wakubwa wa karne ya 20, wakati viongozi wa mataifa 70 wakihudhuria maziko yake.

Mshindi huyo wa tuzo ya Nobel, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili na rais wa Israel, alifariki dunia jumatano akiwa na umri wa miaka 93. Mazishi yake yanahudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Tony Blair na Prince Charles.
 Rais wa zamani wa Marekani akitoa heshima zake za mwisho kwa kushika jeneza lenye mwili wa Simon Peres
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akitoa heshima zake za mwisho
kwa kushika jeneza lenye mwili wa Simon Peres
 Binti wa Shimon Peres akiliwazwa na wanafamilia wakati wa mazishi
 Msiba wa Peres umewakutanisha kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas na Benjamin Netanyahu kama inavyoonekana wakipeana mikono

No comments

Powered by Blogger.