RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA MSAADA WA TSH.MILIONI 545 KUTOKA SERIKALI YA INDIA KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI LILILOTOKEA MKOANI KAGERA
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Serikali ya India kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Wakwanza (kushoto) ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima wakishuhudia tukio hilo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam.Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mfano wa hundi hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya aliyeiwasilisha kwa niaba ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ili fedha hizo zitumike kuwasaidia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana na jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea msaada huo wa fedha kutoka Serikali ya India, Ikulu jijini Dar esSalaam. PICHA NA IKULU
Post a Comment